24.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 22, 2021

Klopp aponda usajili wa Ronaldo

KOCHA wa Liverpool, Juergen Klopp, amesema usajili wa
Cristiano Ronaldo aliyetokea Juventus hauwezi kuisaidia
Manchester United kwa muda mrefu.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 36, alikuwa akihusishwa
zaidi na Manchester City lakini ghafla amerejea Man
United, klabu aliyoiacha mwaka 2009 na kuelekea Real
Madrid.

Huku ikielezwa kuwa nahodha huyo wa timu ya taifa ya
Ureno amepewa mkataba wa miaka miwili, Klopp anasema
Ronaldo ni mchezaji wa muda mfupi, hivyo miaka
michache ijayo Man United itaingia sokoni kusaka mrithi
wake.

Akilizungumzia hilo, Klopp raia wa Ujerumani amesema:
“Si mbaya lakini itachukua miaka miwili au mitatu tu
kuanza kutafuta mrithi wake…”

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,740FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles