31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Kleyah: Lugha ya Kiswahili inavutia kwenye muziki

bg1NA CHRISTOPHER MSEKENA

MKALI wa wimbo wa ‘Msobe Msobe’, Claire Pamela Kamahoro ‘Kleyah’ ameweka wazi kwamba wasanii wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kupata mafanikio kimataifa kwa kuwa lugha ya Kiswahili wanayoitumia katika nyimbo zao inapendwa na watu wa mataifa mbalimbali.

Msanii huyo katika wimbo huo aliomshirikisha mkali wa sauti, mpigaji vyombo mbalimbali vya muziki nchini na mmiliki wa studio ya High Table Sound, Barnaba Elias ‘Barnaba Boy’, umezua mengi huku wengi wakimfananisha na msanii mwenzake, Vanessa Mdee, kutokana na umaridadi wa uimbaji na unenguaji wake.

Kutokana na kupenda muziki, Kleyah aliyeamua kuacha kazi UNDP kwa sababu ya kuendeleza muziki wake. Jana alitembelea ofisi za New Habari (2006) Ltd, zinazochapisha magazeti ya Mtanzania, The African, Bingwa, Dimba na Rai na kuzungumza na waandishi wa magazeti hayo kuhusu muziki na maisha yake kwa ujumla.

“Naamini muziki wangu wa ‘Msobe msobe’ pamoja na sauti yangu nzuri utanisaidia kuwa wa pekee katika muziki wangu na kunifikisha mbali kimataifa, lakini pia kunitambulisha vema hapa Tanzania,’’ alieleza Kleyah.

Kabla ya wimbo wa ‘Msobe Msobe’, nyimbo mbili za msanii huyo, ukiwemo ‘Lovers Eyes’ na ‘Don’t Sly me’ alizozirekodia nchini Afrika Kusini hazikuweza kuteka soko la Afrika Mashariki, licha ya kufanya vizuri katika chati za muziki nchini Afrika Kusini.

“Kutokufanya vizuri kwa nyimbo hizo ndiko kumenirudisha  Tanzania nikafanya wimbo wa ‘Msobe msobe’ ili niweze ku ‘win’ soko la Afrika Mashariki, kwa kuwa kutoka kimuziki hapa ni rahisi kuliko ukiwa nchi nyingine za Afrika Mashariki,” alieleza Kleyah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles