LONDON, ENGLAND
KIUNGO wa Arsenal, Santi Cazorla, atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu kutokana na kusumbuliwa na goti.
Mchezaji huyo alipata maumivu ya goti katika mchezo dhidi ya Norwich, ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.
Hata hivyo, Cazorla alionekana kuwa imara katika dakika zote 90 za mchezo huo, japokuwa alikuwa tayari ameumia goti, ila baada ya kumalizika kwa mchezo hali ilionekana kubadilika.
Klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja hadi Machi, mwakani kutokana na tatizo hilo.Â
Cazorla anaongezeka katika kikosi cha Wenger chenye wachezaji majeruhi ambao ni pamoja na Danny Welbeck, Jack Wilshere, Francis Coquelin na Alexis Sanchez.
Hata hivyo, kikosi hicho kwa sasa kitapewa nguvu na nyota wake ambao walikuwa majeruhi, Aaron Ramsey na Alex Oxlade-Chamberlain, wakati huo Theo Walcott hali yake ikiendelea kuwa nzuri ambapo anaweza kuwa benchi kesho akiungana na Mikel Arteta kwenye mchezo dhidi ya Sunderland.Â