25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

KKKT WAMUOMBA JPM AKAMILISHE KATIBA MPYA

Askofu mpya  wa kanisa la  kiinjili la  kilutheri  Tanzania  (KKKT)  dayosisi ya  Iringa mchungaji Blaston  Gavile kulia  akiongoza  maandamano  ya  maaskofu wa kanisa  hilo nchini  kuelekea uwanja  wa  Gangilonga katika   ibada ya  kuwekwa  wakfu kwake na msaidizi  wake  Himidi  Sagga Picha na Francis Godwin

Na FRANCIS GODWIN-IRINGA 

ASKOFU mpya wa  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, amemuomba Rais Dk. John Magufuli kumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ulioachwa na mtangulizi wake.

Akizungumza baada ya kuwekwa wakfu Askofu Gaville na msaidizi  wake, Himidi  Sagga, katika ibada iliyofanyika  juzi  katika Viwanja  vya  Shule ya Msingi, Gangilonga, alisema Wakristo na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na Serikali ya Dk. Magufuli na ni matarajio yao kwamba mchakato wa kuandika Katiba mpya utamalizwa kama lengo lilivyokuwa.

Askofu huyo alisema Dayosisi ya Iringa inatoa mwaliko kwa vyama vyote vya siasa na jamii nzima ya Watanzania kuendeleza kukuza tunu ya ushirikiano na moyo wa kizalendo ili kuwa na maendeleo yenye tija kwa wananchi na Taifa  kwa  ujumla.

Katika ibada hiyo, Askofu Gaville alieleza kuwa wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dk. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote na

kwa kufanya hivyo, ni  faraja  kubwa kwa  vizazi vya sasa na vijavyo.

“Kweli nasema nchi yetu ina wanyonge wengi kuliko wenye nguvu, tunatiwa moyo na rais na Serikali yake tunapoona wanatetea wanyonge,” alisema Askofu Gaville.

Hata hivyo, askofu huyo aliiomba Serikali iangalie upya suala la kodi kwa mashirika ya dini kwakuwa  baadhi ya kodi wanazolipa ni kwa kuendeleza elimu kupitia vyuo vya ufundi.

“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali, kanisa linasaidia watoto masikini wapate haki yao ya elimu, tunaomba Serikali isituingize katika kundi la watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo kwa sababu wanasoma shule binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles