CUF WATAKIWA KUTOMJADILI PROFESA LIPUMBA

0
422

Na ASHA BANI,

WANACHAMA wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, wametakiwa kutomjadili  Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahimu Lipumba.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa chama hicho, Salim Bimani, imewataka viongozi wa CUF, wanachama na wapenda mabadiliko nchini, kumpuuza Lipumba kwa kile walichosema anatumiwa na baadhi ya viongozi.

Katika maelezo hayo, Bimani alisema wamepokea taarifa za kusajiliwa kwa bodi feki ya Lipumba na baadaye Juni 24, mwaka huu, Lipumba alikaririwa akisema anataka kuwahoji Maalim Seif, Nassor Mazrui (Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar) na viongozi wengine wa chama hicho.

“Tunapenda kuwajulisha wanachama na viongozi wetu wote wa chama, wabunge, madiwani, viongozi wa halmashauri zote, wenyeviti wa mitaa, vijiji, vitongoji, wapenda mabadiliko na Watanzania kwa ujumla, kuwa CUF kupitia vikao halali vya chama, vilishafanya uamuzi juu ya Lipumba na wenzake, kwamba huyo si mwenyekiti tena.

“Anachokifanya Lipumba ni mwendelezo wa kuhakikisha dhamira yake ya kutaka kuivuruga CUF inatimia ili kuzuia haki na uamuzi wa Wazanzibari walioufanya Oktoba 25, mwaka 2015, haipatikani.

“Kwa ujumla, CUF na viongozi wake wamejipanga vema kukabiliana na usaliti huo na hakuna kiongozi au mwanachama yeyote atakayekwenda kuhojiwa na Lipumba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here