Kisa mapaparazi, Kylie apata ajali

0
865

kylie-jennerLOS ANGELES, MAREKANI

MPENZI wa mkali wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Tygar, Kylie Jenner, amesema hana urafiki na waandishi wa habari nchini humo kwa kuwa walimsababishia ajali.

Mrembo huyo amesema hana amani kila akiwa katika matembezi yake ya kawaida kwa kuwa waandishi wa habari wanamzonga mara kwa mara.

Hata hivyo, mwezi uliopita alikutana na waandishi wa habari akaanza kuwakimbia na gari yake na kusababisha ajali wakati anawakimbia waandishi hao.

“Siwezi kuwa na urafiki na waandishi wa habari, wananifuatilia sana, mwezi uliopita nilipata ajali mbaya ya gari kwa kuwakimbia wao, hivyo ninawachukia kwa kiasi kikubwa kwa kuwa hawana heshima, lakini ninakubali kile wanachokifanya ila wanatakiwa kuniheshimu ili tuheshimiane,” alisema Kylie.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here