Kourtney Kardashian anaswa na mtoto wa P. Diddy

0
901

Quincy-Combs-Kourtney-Kardashian-MainNEW YORK MAREKANI

 DADA wa Kim Kardashian, Kourtney, amewashangaza watu baada ya mrembo huyo kuonekana kona mbalimbali akiwa na mtoto wa P. Diddy.

Awali mrembo huyo alionekana mara kwa mara akiwa na Justin Bieber mwenye umri wa miaka 22 na kuwaacha watu wakiwa na maswali mbalimbali ambayo yalikosa majibu, lakini wiki iliyopita mwanadada huyo ameonekana akiwa na Quincy Brown mwenye umri wa miaka 24.

Inasemekana kuwa mwanadada huyu mwenye miaka 36, anapenda kuwa na uhusiano na vijana wenye umri mdogo, lakini haijafahamika kama ni kweli anatoka na mtoto wa P. Diddy.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba kuna picha zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonesha wawili hao wakiwa katika mazingira ya kutatanisha ambapo inaonesha wazi wana uhusiano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here