25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Kisa cha msichana aliyegeuzwa mke na baba yake

Emma Burt akiwa na mtoto wake.
Emma Burt akiwa na mtoto wake.

EMMA Burt (19) amevunja ukimya na kueleza namna baba yake mzazi alivyokuwa akimlisha dawa za kulevya na kumbaka kila siku kwa miaka miwili huku akimtania kwa kumwita ‘mke wangu.’

Mkasa huo ulitokea nchini Uingereza ambapo tayari baba huyo Christopher Wayne Edwards (40) ameshahukumiwa kwenda jela kwa miaka 12 kwa makosa kadhaa yanayohusiana na ngono.

Emma anasema alikutana na mkasa huo alipohamia kwa baba yake Desemba 2012 akiwa na umri wa miaka 15 baada ya kukwaruzana na mama yake mzazi.

Baba huyo alianza kumwonyesha vitendo vya ukatili katika kipindi cha mwezi mmoja wa mwanzo na baadaye akaanza kumwingilia baada ya kupoteza fahamu kwa kuvutishwa bangi.

Hadi anatoroka nyumbani kwa baba yake tayari Emma alishaathirika kwa bangi na dawa za kulevya aina ya cocaine ambazo baba yake alikuwa akimpatia kabla ya kumwingilia.

Emma ameamua kujiweka wazi kwa kuongea baada ya baba yake kuhukumiwa kwa kumbaka na makosa mengine manne ya kufanya mapenzi na mwanafamilia.

Pia alihukumiwa kwa kosa la kukutwa na picha chafu za mtoto na makosa mengine matatu ya kupiga picha chafu na kosa la kumpa dawa za kulevya.

“Katika kipindi cha miezi miwili ya awali akiwa ananifanyia unyanyasaji sikuwa najua alivyokuwa akinibaka na hakuwahi kuniambia,” anasema Emma na kuongeza:

“Alikuwa anasubiri hadi nikiwa nimelala au nakaribia kulala ananiwekea dawa za kulevya na alianza kufanya hivyo mwezi wa tatu tangu nihamie kwake na akawa anaendelea na vitendo hivyo.

“Ilifika wakati nikawa tegemezi wa dawa za kulevya. Sikuwa najua kinachoendelea kwa sababu nilikuwa sijitambui.

“Ilifika wakati nikawa tegemezi wa dawa za kulevya na kusababisha madhara makubwa baada ya kutoroka, sikuwahi kumwambia mtu lakini watu walianza kujua kuwa nilikuwa tofauti, alipenda kunitania kwa kuniita mke wake… kumbe ni kweli ilikuwa hivyo kwa vitendo,” anasema.

Baba huyo alianza kwa kumpa dawa za kulevya za kawaida na baadae akawa anampa dawa kali za daraja A na B.

Emma anasema: “Hivyo ndivyo nilivyozoea awa kama inavyotokea kwa watumiaji wengine.

“Kadiri nilivyotumia, ndivyo nilivyoweza kukataa yaliyokuwa yanatokea.”

Emma alianza kupata matatizo ya akili na kumsababisha Desemba 2014 kujitupa darajani kwa kile alichodai hakutaka kuendelea kupata maumivu.

Emma anaongeza: ” Hapo ndipo nilipoona kuna umuhimu wa kusema kitu.”

Alitoroka nyumbani akiwa na mika 17 baada ya kugombana na familia na ndugu zake wakaita polisi.

Msichana huyo ambaye alikuwa na ndoto za kuwa mfanyabiashara aliona kuongea itawapa hamasa waathirika wengine wa vitendo vya ukatili wa kingono kutoka na kusema yanayowakumba.

Emma anasema: “Naamini kwa kusema aliyokuwa ananifanyia kutawaokoa wasichana wengine.

“Nina binti na nataka niongee na mabinti kama yeye na kuwaambia kwamba wasikubali kupata maumivu niliyoyapata.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles