Magonjwa ya kitambi yanayowatesa wanawake

0
1260

80d6202f6816055848524c15d0835f0f877b8c43

WAGONJWA wenye PCOS wapo hatarini kupata ugonjwa wa kisukari maana wote huwa wana kiwango kikubwa cha insulin kupita kiasi kwenye damu.

Seli za miili yao huwa haziwezi kubaini uwepo wa insulin kwenye damu na hivyo insulin huwa haifanyi kazi yake ipasavyo.

Na hali hii ya seli za mwili kutoweza kubaini uwepo wa insulin kwenye damu inasababisha sukari katika damu kutofanyiwa kazi na hatimaye sukari inaanza kupanda na kukupelekea kupata kisukari.

Hali ya sukari kwenye damu kuwa katika kiwango cha juu muda wote na kiwango hiki kingi cha insulin ndicho kimekuwa kichochezi kikubwa kwa wanawake wengi kuugua ugonjwa huu.

Kinachosababisha insulin kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi

Neno Insulin resistance limekuwa likitafsiriwa tofauti sana na watu wengi hasa washauri wa afya. Lakini tafsiri mbaya kabisa ambayo watu wengi wanayo ni kwamba insulin inaposhindwa kufanya kazi maana yake mafuta mabaya yameziba kwenye kipokea insulin na hatimaye insulin haiwezi tena kufanya kazi. Huu ni uongo tena ulio wazi.

Kila mtu anajua jiji la Dar es Salaam lilivyo na joto kali kupita hali ya hewa ya mikoa mingine yote, mtu ambaye ni mkazi wa Mwanza ukimleta Dar es Salaam ni lazima atasumbuka sana kuzoea joto hili.

Na ndio maana baada ya kukaa miezi sita anakuta amezoea mazingira anaona kama hakuna utofauti kabisa.

Pia chukulia mfano mlevi wa pombe kali mwanzo alikuwa anakunywa chupa mbili na analewa sana hadi kuendesha gari hawezi, lakini kadiri muda unavyoenda atajikuta anapiga pombe bila kulewa chochote kabisa.

Maana yake zile chupa mbili zimemzoea haziwezi tena kumlewesha kama zamani.

Mfano wa mwili ni pale unapoambiwa na washauri wa afya usitumie ‘antibiotic’ ovyo maana wale wadudu watazoea dawa na hatimaye isiwe rahisi kuwatibu.

Ndio maana tunaambiwa tupime kwanza kabla ya kunywa dawa ili kupunguza matumizi ya dawa ovyo na kusababisha dawa zingine kutokuwa na uwezo wa kuangamiza vimelea.

Hivyo basi hata kongosho la binadamu linapomwaga maji ya insulin kwa kutumia seli zake aina ya beta moja kwa moja kwenye damu, kadiri linavyozidi kuongeza kiwango chake kingi katika damu ndivyo itafikia hatua seli za mwili zinapata ‘Insulin Tolerance’ yaani hiyo insulin haiwezi tena kufanya kazi yake ipasavyo.

Hivyo kisababishi cha insulin resistance au Tolerance ni insulin yenyewe.

Ulaji wa vyakula vya wanga kupindukia na vyakula vyenye sukari vinasababisha kiwango cha insulin kumwagwa kwa wingi kupita kiasi na hatimaye kupelekea insulin kuwa katika kiwango cha juu muda wote na mwishowe insulin inakuwa haiwezi tena kufanya kazi yake.

Kwa hiyo basi chanzo kikubwa cha insulin kuwa katika kiwango cha juu kupita kiasi ni ulaji wa vyakula vya wanga na sukari kupita kiasi.

Na tafiti zinaonesha kwamba vyakula vya wanga na sukari vinaongoza kupandisha kiwango cha insulin mwilini mwako, ikifuatiwa na vyakula vya protini na vyakula vya mafuta vimeonesha havina madhara kabisa ya kuongeza insulin katika damu baada ya kula.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here