24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kisa Bieber… Selena Gomez ajiongezea maadui  

selena-gomez-gq-0516-01Na BADI MCHOMOLO

NI miaka miwili sasa tangu msanii wa Pop nchini Marekani, Justin Bieber kuachana na mpenzi wake Selena Gomez, hakika ulikuwa ni uhusiano ambao ulikuwa unazungumziwa na mitandao mbalimbali ya kijamii.

Uhusiano wao ulikuwa na jina kubwa kutokana na wawili hao kuonesha wazi mapenzi yao huku wakiwa na umri mdogo, hata hivyo mkali huyo wa muziki wa Pop alikuwa anatamba na wimbo wake wa ‘Baby’ ambapo mashabiki wengi wakidai kuwa ulikuwa maalumu kwa ajili ya mpenzi wake.

Lakini siku zote fahali wawili hawawezi kuishi zizi moja, hivyo ndivyo ilivyo kwa maisha ya wawili hao, kwa kuwa wakati huo wanaachana, Bieber alikuwa katika ubora wake, wakati huo Selena naye anafanya muziki na mitindo.

Lakini inadaiwa kwamba Bieber alijiona kuwa bora zaidi ya mwenzake, hivyo kutokana na umri wake kuwa mdogo alikuwa anatamani kutembea na warembo mbalimbali, hivyo Selena naye akaona bora awahi kuvunja uhusiano ili kuonesha kuwa anaweza kuchukua uamuzi mgumu.

Hata hivyo Selena alifanya hivyo huku akiwa anampenda Bieber, ila alikuwa hana jinsi. Kitendo hicho kilimtesa sana Selena hasa baada ya kuona kuwa Bieber hana mpango wowote wa kutaka kurudiana na yeye anashindwa kuomba kurudiana.

Wiki iliyopita Bieber aliamua kuweka wazi uhusiano na mpenzi wake mpya Sofia Richie, ambaye ni mtoto wa mkongwe wa muziki nchini Marekani, Lionel Richie. Ni wazi kuwa kitendo hicho kilimpa wakati mgumu Selena kwa kuwa anaona hana tena nafasi katika penzi la mkali huyo wa muziki wa Pop.

Katika utambulisho ambao Bieber aliufanya, baadhi ya mashabiki walionesha chuki kwa kitendo hicho na walidaiwa kuwa ni wale ambao wanaungana na Selena na waliamini kuwa ipo siku wawili hao watakuwa pamoja.

Mashabiki walimtukana msanii huyo kwenye mitandao ya kijamii kwa kitendo cha kumtambulisha mpenzi wake na kufikia hatua msanii huyo kuamua kujitoa kwenye akaunti yake ya Instagram na kusema kuwa watu wasimfuatilie maisha yake.

Selena alionekana kuwa na furaha na kuandika kwenye akaunti yake ya Instagram kwamba kama anataka watu wasimfuatilie maisha yake basi asiwe anaweka picha za wapenzi wake kwenye mitandao.

Kauli hiyo ya Selena ilionesha kuleta utata kwa baadhi ya mashabiki kwa kuwa wapo ambao walimshambulia na kudai kwamba mrembo huyo bado anampenda Bieber na ndiyo maana anamfuatilia.

Hata hivyo Bieber hakuonesha dalili yoyote ya kutaka kumjibu Selena, hivyo baadhi ya mashabiki wa Bieber walionekana kumshambulia mrembo huyo kwa matusi kwa lengo la kulipa kisasi kama ilivyo kwa Bieber baada ya kumtambulisha mpenzi wake mpya Sophia Richie.

Kwa kitendo hicho tayari Selena ameanza kupoteza baadhi ya mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii ambao wameonesha kuwa hawana mpango wa kuendelea kuwa rafiki na msanii huyo kwa kuwa anafanya vitu vinavyochochea ugomvi.

Charlie Puth ambaye ni mtayarishaji mkubwa wa muziki nchini Marekani, ameweka wazi kujitoa urafiki na Selena kwenye akaunti ya Instagram kutokana na kitendo kinachoonesha kuwa kinaweza kusababisha mgogoro mkubwa na prodyuza huyo alikuwa na mpango wa kufanya kazi na Selena hivi karibuni.

Hata hivyo Selena ametambua kosa lake na kupitia akaunti hiyo ya Instagram, ameomba radhi kwa mashabiki wake kutokana na kitendo cha kuijibu kauli ya Bieber, lakini ukweli ni kwamba ameanza kupoteza mashabiki kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles