KING MAJUTO AOMBA MSAADA

0
1171

Na JEREMIA ERNEST


MWIGIZAJI na mchekeshaji mkongwe, Amri Athumani ‘King Majuto’, anawaomba wasanii na wadau wa sanaa kumsaidia kufanikisha matibabu yake ya nyonga.

Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu sasa na matibabu yake yanafanyika katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA, Mzee Majuto ameomba kusaidiwa kufanikisha matibu yake kwa njia ya maombi pamoja na fedha.

“Watanzania waniombee niweze kurudi katika hali yangu, pia wanisaidie kukidhi gharama za matibabu, lakini kwa sasa hali yangu inaendelea vizuri,” alisema Majuto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here