29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Kimei: Nitatumia elimu, uzoefu wangu kuibadili Vunjo

Na Upendo Mosha, Moshi

MGOMBEA ubunge kwa tiketi ya chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Vunjo, Charles Kimei, amewaahidi wananchi kutumia elimu aliyonayo na utashi wake katika masuala ya uchumi kuleta maendeleo yaliotukuka katika Jimbo Hilo iwapo watamchagua.

Akizungumza baada ya kufanyiwa tambiko la kimila la jamii ya kimasai la kumtaki baraka kwa Mungu katika harakati zake za kuwa mbunge wa jimbo hilo, katika Kijiji cha Mawala Kata ya Kahe Magharibi, kimei alisema anauwezo wa kuwaletea wananchi hao maendeleo iwapo watamuamini na kumchagua.

“Nilipokuwa CRDB nilitumia mikakati kikubwa na ubunifu wa hali ya juu kuifanya benki Ile iaminike na mimi nataka niwaahidi ndugu zangu mkinichagua kuwa mbunge wenu, nitatumia raslimali ya watu nilionao ambao wananiamini kuleta maendeleo katika jimbo letu haswa katika ukandaa huu wa tambarare ambao unaonekana kusahaulika,”alisema.

Alisema atatumia mtandao wa mahusino alionao kupata fedha na raslimali nyingine kuwekeza katika maeneo ya ukanda wa chini ikiwemo katika sekta ya afya, elimu na miundombinu ya barabara pamoja na umeme.

Aidha alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, tathimini inaonyesha hakuna hatua yeyote ya maendeleo iliyopigwa katika jimbo hilo katika maeneo yote ya milimani na tambarare jambo ambalo yeye hatokubali iwapo atakuwa mbunge.

“Hatua ya maendeleo katika Jimbo la Vunjo ni ndogo sana ikilinganishwa na maeneo mengine katika nchi yetu, katika eneo hili hakuna hata kituo kimoja cha afya kilichojengwa na katika elimu shule pia ni changamoto kubwa, nitahakikisha hivi vyote navipigania.

“Huu ni wakati wa kutathimi na kuona maendeleo ya kweli yanatokana na CCM na niwaahidi nitaanza kutekeleza baadhi ya changamoto zinazo wakabili, naomba mniamini na mnitume nitumike kwenu ipasavyo,”alisema Kimei.

Awali akitekeleza zoezi hilo la kimila Leigwanani, Loshiro Ngablada, alisema jamii hiyo kupitia wazee wa kimila wamekutana na kuona ni wakati muafaka wa kumfanyia tambiko hilo la kimila linaloashiria ushindi kwani ndio kiongozi pekee wanayemuamini kwamba atawaletea maendeleo.

“Zoezi hili tumelifanya kwa unyenyekevu wa hali ya juu, tunalifanya sisi na pia tumeomba Mungu, tunaamini wewe ndio pekee wa kutuletea maendeleo kwani kwa zaidi ya miaka mitano toka tumekuwa na Mbunge wa upinzani amekuwa na ahadi zisizotekelezeka,”alisema.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mawala, Devid Laiza, alisema kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme, kituo cha afya na barabara na kwamba wanamuomba mgombea huyo iwapo atashinda akumbuke changamoto hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles