Kim kumsapoti Kanye kugombea urais

0
2285

LOS ANGELES, MAREKANI 

MKE wa rapa Kanye West, Kim Kardashian, ametumia ukurasa wake wa Twitter na kusapoti harakati za mume wake huyo kugombea urais nchini Marekani.

Tangu mwaka jana rapa huyo alidai yupo kwenye maandalizi ya kugombea urais, lakini mke wake hakuwa kati ya watu ambao wanasapoti mipango hiyo, ila kwa sasa Kim amejitokeza na kuonesha sapoti yake.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 39, alitumia Twitter na kurudia posti ya maneno ambayo aliyaandika Kenye wiki iliopita juu ya kutaka urais mwaka huu, mbali na kuposti maneno hayo pia aliongeza picha mbalimbali ikiwa pamoja na bendera ya Marekani.

Kim ambaye amefanikiwa kupata watoto wanne na rapa huyo, alikuwa hana furaha kuona mume wake anajiingiza kwenye siasa, lakini kwa sasa amempa baraka zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here