Rihanna kuuweka muziki pembeni

0
2183

NEW YORK, MAREKANI 

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Rihanna Fenty, ameweka wazi kusitisha mipango yake ya kuachia albamu ya tisa na kujikita kwenye mambo ya urembo.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 32, mara ya mwisho kuachia albamu ilikuwa 2016, lakini kulikuwa na taarifa kwamba mwaka huu ataachia albamu mpya kutokana na uhitaji wa mashabiki zake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la nchini Uingereza, msanii huyo amedai mipango hiyo ya muziki anaiweka pembeni na kujikita kwenye vifaa vya urembo kwa kuwa anaamini ndio biashara inayoweza kumfanya kuwa bilionea tofauti na muziki.

“Najua mashabiki wanasubiri albamu ya tisa, lakini ukweli ni kwamba tunaiweka pembeni na kujikita kwenye urembo, hii ni sehemu ambayo inaweza kunifanya kuwa bilionea kwa sasa, lakini muziki bado upo pale pale,” alisema Rihanna.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here