22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

KIM KARDASHIAN: SIKUCHAGUA JINA LA CHICAGO

NEW YORK, Marekani


STAA Kim Kardashian, amesema kwamba, hakutaka kumpa jina la  Chicago mwanawe, badala yake alitaka kumbatiza la bibi yake.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 na mumewe, Kanye, walimbatiza mtoto huyo Januari 15, mwaka huu baada ya kuibuka mvutano kuhusu jina.

Mbali na mtoto huyo, Kim na Kanye, wana watoto wengine wawili ambao mkubwa wa kike ana umri wa miaka minne anayeitwa North na wa kiume, Saint.

Akizungumza katika kipindi maalumu, staa huyo alisema tayari alikuwa ameshachagua majina mawili kabla ya kumpachika jina hilo.

“Nilitaka kumwita Jo kwa sababu ya bibi yangu Mary Jo ama Grace, lakini baadaye ndio tukaafikiana kumwita  Chicago,” alisema nyota huyo katika mahojiano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles