31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

MTOTO WA SERENA AANZA KUVUTIWA NA TENISI

NEW YORK, Marekani


NGULI wa tenisi kwa upande wa wanawake, Serena Williams, amesema kwamba binti yake hawezi kupepesa macho wakati anapokuwa akiangalia wacheza tenisi uwanjani.

Kwa mujibu wa nyota huyo, binti huyo mwenye umri wa miezi saba,  Alexis Olympia, mara kwa mara amekuwa akimwangalia kwa makini pindi anapokuwa uwanjani na kwamba hata pia hawezi kufumba macho, wakati mchezo huo unapokuwa ukionyeshwa katika televisheni.

“Anaangalia mchezo wa tenisi kama tai. Hawezi kufumba jicho wakati mchezo unaendelea,” alisema mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 36.

Mbali na kumzungumzia mwanawe, staa huyo pia alielezea jinsi alivyojisikia baada ya kubaini kuwa ni mjamzito akisema kwamba, alikuwa akifahamu pengine ndio mwisho wa kibarua chake hicho.

Hata hivyo, alisema tofauti na alivyotarajia anaona hali yake ipo kama kawaida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles