Kim Kardashian aibiwa vito vya thamani ya dola milioni 10

0
713

kim-kardashian-net-worth

PARIS, Ufaransa

POLISI jijini Paris nchini Ufaransa, wamesema mke wa  msanii wa hip hop, Kanye West, Kim Kardashian, ameporwa vito vya thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 10 na watu waliokuwa na silaha akiwa amepumzika katika makazi yake jijini hapo.

Mwanadada huyo aliibiwa vito hivyo baada ya kuvamiwa sehemu alipokuwa amepumzika, watekaji walimfunga kamba kisha wakamfungia bafuni na baada ya kumwibia, walitoweka eneo la tukio.

Msemaji wa mwanamama huyo, alisema Kim alikuwa katika Jiji hilo kwa ajili ya kuhudhuria maonyesho ya wiki ya Fashion yaliyokuwa yakifanyika jijini humo.

“Hakuumia sehemu yoyote, alishtuka tu baada ya uvamizi huo na kuibiwa vito vyenye thamani hiyo, lakini yupo vizuri na anaendelea vyema,” alieleza msemaji wake.

Polisi walieleza kwamba watekaji hao watano waliiba boksi lenye vito vya thamani ya euro milioni 6 sawa na dola milioni 6.7 na pete yenye thamani ya euro milioni 4.

Wakati tukio hilo likitokea, mume wa mwanadada huyo, Kanye West, alikuwa jukwaani kwenye tamasha la muziki na sanaa lililokuwa likifanyika jijini New York, Marekani ambapo alilazimika kukatisha shoo yake huku akiwaomba radhi mashabiki wake kutokana na hilo.

“Samahani nimepatwa na taarifa za tatizo kwa familia yangu, hivyo nasimamisha shoo,” Kim aliwaeleza mashabiki wake.

Kim alishawahi kukutana na matukio ya kuvamiwa ambapo mwaka 2014, aliwahi kuvamiwa lakini pia hivi karibuni aliwahi kuvamiwa na shabiki wake na kutukanwa alipokuwa akiingia katika moja ya mgahawa nchini Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here