25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Benki ya Dunia yaisifia Tanzania kwa kuhakikisha usawa

wb

Benki ya Dunia imeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa mataifa machache duniani ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo inayohusu usawa duniani, Tanzania ni moja ya nchi tatu zilizotajwa kufanya vizuri. Nchi nyingine ni Cambodia na Brazil kama nchi tatu zilizopiga hatua sana.

Ripoti hiyo inasema, nchini Tanzania, ufanisi ulipatikana katika kipindi ambacho taifa hilo lilipata ukuaji thabiti wa uchumi wa kiwango cha wastani cha asilimia 6.5 kila mwaka kati ya 2004-2014.

“Kiwango cha umaskini kitaifa kilishuka kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi asilimia 28.2 mwaka 2012,” ripoti ya benki hiyo inasema.

Kwenye kipimo cha pengo kati ya maskini na matajiri, Tanzania iliimarika kutoka alama 39 mwaka 2007 hadi chini ya alama 36 mwaka 2012.

Kipimo cha wastani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara mwaka 2015 kilikuwa alama 45.1.

“Hatua zilizopigwa na Tazania katika kupunguza pengo kati ya maskini na matajiri kipindi hiki kifupi ni cha kutia moyo,” Benki ya Dunia inasema.

“Ushahidi unaonesha ufanisi huu ulitokana sana na ongezeko la matumizi miongoni mwa watu wa tabaka la chini.”

Miongoni mwa asilimia 40 maskini, matumizi yaliongezeka kwa asilimia 3.4 ikilinganishwa na asilimia 60 wenye pesa ambao ongezeko lao la matumizi lilikuwa asilimia 1 pekee.

“Ni wazi kwamba mambo yaliwaendea vyema zaidi watu maskini kuliko matajiri kipindi hiki,” ripoti hiyo inasema.

Kuanzia mwaka 2007, kulikuwa na ongezeko katika biashara ya rejareja na viwanda, hasa vya vyakula, vinywaji na tumbao jambo ambalo benki hiyo inasema liliwezesha watu wasio na ujuzi sana kushiriki katika uchumi.

Kujitolea kwa serikali katika kuendeleza sera ambazo zinalenga kusawazisha mapato pia kumechangia Tanzania kupiga hatua, benki hiyo inasema. (Source BBC)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles