28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kilombero: Hakutakuwa na uhaba wa sukari mwezi wa Ramadhani

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Sukari ya Kilombero chini ya chapa ya “Bwana Sukari” inapenda kuwatoa hofu wananchi, hususan wapenzi na watumiaji wa sukari ya Kilombero “Bwana Sukari” kuhusu upungufu wa sukari katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Aprili.

Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero, Fimbo Butallah akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kulia ni Meneja Mauzo Harshid Chavda na kushoto ni Meneja Usambazaji Johannes Rugalema.

Hayo yameelezwa leo Machi 24, 2022 na Mkuu wa Idara Biashara, Fimbo Butallah, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Tamko hilo limekuja kutokana na historia ya kupanda kwa bei za bidhaa nyingi za vyakula kila uanzapo mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusababisha adha kubwa kwa wananchi, hususan waumini wanaofunga katika mwezi huo.

Kutokana na hilo, kampuni ya Sukari ya Kilombero imewasihi wafanyabiashara wote, wa jumla na rejareja wanaouza bidhaa za “Bwana Sukari” kutopandisha bei, jambo ambalo limekuwa likiwakandamiza watumiaji wa sukari ambapo matumizi yake huongezeka zaidi katika mfungo wa Ramadhani.

Fimbo amesema, “Tunafahamu kuwa katika uchumi wa soko huria, sisi kama wazalishaji haturuhusiwi kuwapangia wafanyabiashara bei ya kuuza bidhaa. Hata hivyo tunao wajibu mkubwa wa kuwashauri kuhusu upandishaji holela wa bei, haswa pale ambapo sisi kama wazalishaji wa sukari hatujapandisha bei ya bidhaa hiyo. Tunawasihi wafanyabiashara kote nchini kutopandisha bei za sukari katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuepuka taharuki inayoweza kujitokeza,” amesema Fimbo.

Akizungumzia suala la uhaba wa sukari ambao mara nyingi hujitokeza katika mfungo wa Ramadhani, Fimbo alisema kuwa Kampuni ya Sukari ya Kilombero inayo akiba ya kutosha kulivusha taifa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuongezea kuwa tayari kampuni imepata kibali cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ili kuziba pengo la uzalishaji.

“Tumekwishaanza taratibu za uagizaji wa sukari ambayo inatarajiwa kuanza kuingia nchini muda wowote kuanzia hivi sasa. Tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuhusu upandaji holela wa bei ya sukari, hususan chapa ya “Bwana Sukari” kwani kampuni imeandaa mikakati thabiti kukabiliana na tatizo hilo katika msimu huu”, amesema Fimbo.

Kampuni ya Sukari ya Kilombero, ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Illovo Sugar Africa kwa Asilimia 75 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 25 ipo katika maandalizi ya mradi wake wa upanuzi ambao utakuza uwezo wa kampuni hiyo wa kutengeneza sukari na kupunguza uhaba wa sukari nchini kupitia chapa yake ya “Bwana Sukari”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles