26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kikwete: Lowassa ametoa mchango mkubwa kwa Taifa, mema yake hayafutiki

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete amesema Waziri Mstaafu Edward Lowassa ametoa mchango mkubwa katika Taifa na yaliyotokea ni changamoto katika maisha lakini hayafuti mema na mazuri aliyofanya kwaajili ya Nchi.

Kauli hiyo ametoa leo Februari 12, jijini Dar es Salaam na Dk. Kikwete baada ya kufika nyumbani kutoa pole ya msiba nyumba kwa Waziri Mkuu Hayati Lowassa aliyefariki Februari 10, mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Amesema anamfahamu Waziri Mkuu Mstaafu Lowassa kwa mda mrefu wamekuwa pamoja tangu wakiwa vijana na kisha kuwa viongozi hivyo mchango wake ni mkubwa kwa Taifa letu.

“Nimepokea kwa mshituko taarifa ya kifo nilikuwa nafahamu kwamba anaumwa lakini sikutegemea ingefikia hapa ilipofikia na mfahamu Marehem kwa mda mrefu tulikuwa vijana pamoja tulikuwa chuo kikuu pamoja tukatangulia sisi kuingia kwenye chama na baadaye akafuata na tumefanya kazi pamoja kwenye chama kwa muda huo wote,” amesema Dk. Kikwete.

Ameeleza kuwa baadaye aliendelea kwenye shughuli za jeshi mwenzake akaendelea kwenye shughuli za chama na wakawa wabunge na wakafika baraza la mawaziri.

“Mwaka 1995 siku moja asubuh nikapokea ugeni mtoto akaja chumbani akaniambia baba kuna ugeni nikawakuta marafiki zangu watatu kaka yangu Samuel Sitta, Edward Lowassa na Rostam Aziz wakaja wakaniambia kwamba tunataka muende na Edward Dodoma mkachukue fomu ya kugombea urais mimi nikasema jambo hili halipo kwenye mawazo yangu kama yeye lipo kwenye mawazo basi aende naye akasema haendi bila wewe,”ameeleza.

Hayati Edward Lowassa, enzi za uhai wake.

Amesema basi wakabishana hadi walipokubaliana kwamba wacha waende kuchukua fomu hizo wakazijaza zikarudishwa mchakato ndani ya chama ukaendelea mwenzangu hakubahatika yeye alibahatika kuwemo kati ya wale watano na baadaye wakapiga kura NEC akawemo katika wale watatu.

Dk. Kikwete amesema wakaenda kwenye mkutano mkuu akawemo katika wawili lakini kura zake hazikutosha akapatq mzee Mkapa akaja kuwa Waziri wake wa Wizara ya Mambo ya Nje Lowassa akawa waziri tena.

Amesema Mwaka 2005 walipoteuliwa kugombea urais Lowassa akaja kuwa Waziri Mkuu kapata changamoto katikati ikabidi akae pembeni wakaendelea kuwa marafiki na kushirikiana kwa kila liwezekanalo.

Dk. Kikwete ameongeza kuwa ameugua Mwenyezi Mungu amechukua roho yake anachoshauri waendelee kumuombea Mungu aipokee roho yake aiweke mahali pema peponi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles