KIGOGO IPTL MATATANI

0
697

Na JUSTIN DAMIAN - DAR ES SALAAM

BODI ya Wakurugenzi  ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mwendeshaji, Parthiban Chandrasakaran.

Chandrasakaran amesimamishwa kazi kuanzia Februari 12 mwaka huu kwa tuhuma za kutoa maneno ya kashfa dhidi ya wafanyazi na viongozi wakuu wa nchi.

MTANZANIA limepata nakala ya barua iliyoandikwa na bodi ya wakurugenzi ya kampuni hiyo kwenda kwa Chandrasakaran, iliyosainiwa na Katibu wa bodi hiyo, Wakili Joseph Makandege kwa niaba ya mwenyekiti wake.

Barua hiyo imeandikwa baada ya kubainika kwa mpango wa chini kwa chini wa mkurugenzi huyo, raia wa Malaysia kutaka kupunguza wafanyakazi bila kufuata utaratibu, ikiwamo kupata ridhaa ya bodi ya wakurugenzi.

Vyanzo vya kuaminika vya gazeti hili kutoka ndani ya kampuni hiyo, vimeliambia MTANZANIA kuwa Chandrasakaran alianzisha mchakato wa kupunguza wafanyakazi huku akilenga kuwalipa malipo …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here