Kifyatua kombora chanaswa katika begi la abiria uwanja wa ndege

0
686

WASHINGTON DC, MAREKANI

MAOFISA wa usalama wa uwanja wa ndege nchini Marekani, wamekamata kifaa kinachorushia kombora, kikiwa kwenye mzigo wa abiria mjini Maryland.

Chombo hicho kiligundulika kwenye mzigo wa mwanamume mmoja ambaye alisema alikuwa akifanya kazi jeshini.

Aliwaamba maofisa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baltimore/Washington kuwa kifaa hicho kilikuwa zawadi kutoka Kuwait.

Kifaa hicho kimechukuliwa na maofisa wa zimamoto kwa kukiteketeza.

Idara ya Usalama wa Usafirishaji imesema katika taarifa yao kuwa mwanamume huyo mkazi wa Jacksonville, Texas, aliwaambia maofisa kuwa alikuwa mfanyakazi wa jeshi mwenye bidii.

”Bahati, kifaa hicho hakikuwa kikifanya kazi. Kilishikiliwa na kupewa kwa maofisa wa zimamoto kukiteketeza. Mtu huyo aliruhusiwa kuendelea na safari,” taarifa zinaeleza.’

Si mara ya kwanza kwa mamlaka kukutana na matukio ya namna hiyo.

Agosti mwaka jana, maofisa waligundua vifaa mithili ya bomu la kurusha kwa mkono katika begi Uwaja wa Ndege wa Kimataifa wa Newark Liberty.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here