26.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 16, 2024

Contact us: [email protected]

Ndege ya kivita Pakistan yaanguka, yaua 17

Rawalpindi, Pakistan

NDEGE ya kivita ya Pakistan imedondoka eneo la makazi ya watu na kusababisha vifo vya raia 15 na askari watano waliokuwa katika ndege hiyo.

Moto uliotokea baada ya ndege hiyo kuanguka Kijiji cha Mora Kalu, uliteketeza makazi ya baadhi ya wanakijiji.

Askari watatu na marubani wawili, ni miongoni mwa waliofariki dunia katika ajali hiyo.

Maofisa wamesema vifo vinaweza kuongezeka kwa sababu baadhi ya majeruhi 15 hali zao ni mbaya.

“Miili ya marehemu na majeruhi imepelekwa hospitalini, wengi wa majeruhi waliungua na moto uliotokea baada ya ndege kuanguka,” alisema mmoja wa maofisa hao.

Wakieleza tukio hilo, baadhi ya wananchi walisema waliamshwa na mlio mkubwa na baadaye kutoka nje wakaona moto ukiwaka karibu na makazi yao.

“Niliamshwa na sauti ya mlipuko, nilivyotoka nje nikaona moto mkubwa, tukakimbia kwenda eneo la tukio.

“Watu walikuwa wakilia, tulijaribu kuwasaidia, lakini moto ulikuwa mkubwa sana na tukashindwa kufanya lolote, marehemu ni pamoja watu saba wa familia moja ambapo wengi wao waliteketea kwa moto,” Mohammad Sadiq aliambia AFP.     

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Mohammad Mustafa, alisema nyumba ya dada yake iliathiriwa pia na moto huo.

“Dada yangu, mumewe na watoto wao watatu walifariki dunia ndege hiyo ilipoangukia nyumba yao,” Mustafa aliiambia AP akiwa karibu na nyumba ya dada yake iliyoharibiwa na moto.

Abdul Rehman, ambaye ni daktari, alisema nyumba tatu zimeharibiwa na moto na kwamba miili ya marubani imepatikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles