23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wafungwa 57 wauawa gerezani Brazil

Para, brazil

VURUGU kati ya magenge mawili ya gerezani, yamesababisha vifo vya watu 57 ambapo kati yao 16 walikatwa vichwa.

Hayo ni kwa mujibu wa maofisa katika Jimbo la Para, ikiwa ni makabiliano mabaya kabisa ya karibuni wakati Serikali ikipambana kuyadhibiti magereza yaliyojaa kupindukia.

 Vurugu zilianza katika gereza moja la mji wa kaskazini mwa Altamira, zikiyahusisha magenge hasimu.

Wafungwa kutoka genge moja waliwasha moto chumba cha gereza kilichokuwa na wafungwa wa genge jingine.

Taarifa ya Jimbo la Para imesema wengi wa waliuawa katika moto huo huku walinzi wawili wakichukuliwa mateka, lakini wakaachiwa baadaye.

Ghasia za magerezani zimekuwa changamoto kubwa ya usalama Brazil.

Mei mwaka huu, wafungwa 55 waliuawa kwenye mashambulizi gerezani katika jimbo la kaskazini la Amazonas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles