22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Alliance yaanika silaha 28, yamrejesha Tegete

Damian Masyenene, Mwanza

WAKATI dirisha la usajili kwa timu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na la Pili Tanzania Bara limepangwa kufungwa leo, Klabu ya Alliance imeweka wazi majina ya wachezaji wake itakaowatumia msimu ujao.

Mbalia ya kuanika majina ya wachezaji itakaowatumia, pia klabu hiyo ya Mwanza imeanika orodha ya wachezaji ilioachana nao kutokana na sababu tofauti.

Katika orodha hiyo, Alliance imewasajili mshambuliaji mkongwe, Jerrison Tegete ambaye amewahi kutamba na Yanga, Majimaji na Kagera Sugar.Pia imemsajili

mchezaji wao wake wa  zamani, Athanas Mdamu aliyekuwa akikipiga Kariobangi Sharks ya Kenya.

Wengine waliomwaga wino klabu hapo ni  Abdulkarim Hamim, Peter Mwangosi, Erick Murilo, Hussein Kasanga( Mbao FC), Daniel Manyenye (Biashara United), Selia Gambareko (Western Stima, Kenya), Sixtus Mwasekaga (Stand United) na Deusdedith Okoyo aliyejiunga na timu hiyo akitokea
 Geita Gold.

 Mwenyekiti wa Mashindano Alliance, Yusuph Budodi alisema nyota wao 16 wa kikosi cha msimu uliopita wataendelea kuwa nao, huku tisa wakiondoka, ambapo wachezaji wapya 12 wamesajiliwa.

Aliwataja walioachana nao kuwa ni mlinda mlango, Ibrahim Isihaka, Dickson Ambundo, Bigirimana Blaise, Hussein Javu, Jamal Mtegeta, Rajabu Kibera,Mapinduzi Balama, Nteze John na Paul Mahona.

Akizungumzia maandalizi ya timu, Msemaji wa Alliance, Jackson Mwafulango alisema kikosi chao tayari kimeshaanza mazoezi na wameandaa utaratibu wa maandalizi, ambapo wanasubiri pendekezo la benchi la ufundi kuhusu wapi timu ifanyie maandalizi yake na mechi za kirafiki.

Mwafulango alisema nafasi mbili zilizobaki za usajili wanatarajia kuzijaza kwenye dirisha dogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles