KIDUM ANUSURIKA KIFO BURUNDI

0
961

NAIROBI, KENYA


STAA wa muziki nchini Kenya, Jean-Pierre Nimbona, akijulikana kwa jina la Kidum, amenusurika kifo baada ya kugundulika kuwa alikula kitu chenye sumu mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Burundi.

Wiki iliyopita msanii huyo alikuwa nchini Burundi kwenye tamasha la La Francophone, katika Chuo Kikuu cha Bujumbura, hivyo alidaiwa kutumia chakula chenye sumu.

Hata hivyo, baada ya kufanyiwa matibabu jijini Bujumbura, msanii huyo ameruhusiwa na inadaiwa hali yake inaendelea vizuri, lakini bado hajawasili nchini Kenya kutokana na afya yake kuwa dhaifu.

“Nilikuwa kwenye hatari kubwa baada ya kugundulika kuwa nimekula chakula chenye sumu, lakini ninamshukuru Mungu kwa kuwa hali yangu inaanza kukaa vizuri, nawashukuru wote wanaoniombea ili niweze kuwa katika hali yangu ya kawaida,” aliandika Kidum.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here