23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

TYGA AKANUSHA KUZAA NA KYLIE JENNER

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Micheal Stevenson ‘Tyga’, amekanusha taarifa kwamba amezaa na mdogo wake Kim Kardashian, Kylie Jenner.

Tyga na Kylie walikuwa kwenye uhusiano tangu 2014, lakini wakaja kuachana 2017, hivyo mrembo huyo akawa anatoka na rapa Travis Scott na kufanikiwa kupata mtoto mapema mwaka huu, lakini kulikuwa na taarifa kwamba mtoto huyo ni wa Tyga.

“Sijawahi kusema lolote tangu nimeachana na Kylie, lakini nashangaa kuona taarifa kwamba mtoto wa mrembo huyo mimi ndio baba.

“Tafadhali naomba taarifa hizi zisiendelee kusambaa, hasa kwa kumnyooshea kidole mtu au familia, baada ya kuachana kila mtu aliendelea na mambo yake, lakini nashangaa kuona watu wanasambaza vitu ambavyo havina ukweli,” alisema Tyga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles