27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

RICK ROSS ATUMA SALAMU KENYA

NAIROBI, KENYA


RAPA William Roberts II, maarufu kwa jina la Rick Ross, ametuma salamu kwa mashabiki wa muziki wake nchini Nairobi kuelekea tamasha la NRG, litakalofanyika kwenye ukumbi wa Carnivore Grounds, Aprili 28.

Msanii huyo amekuwa akisubiriwa na mashabiki kwa hamu kubwa kwa kipindi cha miaka kadhaa ambacho alikuwa anahusishwa kutaka kufanya shoo moja kubwa, lakini taarifa hizo hazikuwa za kweli, lakini sasa ameamua kuthibitisha kwa kuwatumia ujumbe mashabiki jijini Nairobi.

“Habari gani Nairobi, ni mimi Boss wao Ricky Rozzay, hii itakuwa mara yangu ya kwanza kuja Kenya kwa ajili ya tukio maalumu, Boss Rick Ross nitaungana na mabosi wengine kwenye tamasha la NRG Wave, Aprili 28,” alisema msanii huyo.

Hata hivyo, waandaaji wa tamasha hilo, NRG, wametangaza kiingilio, kiasi cha chini ni Ksh 3,000, ambazo ni sawa na Sh 66,321 za Tanzania, huku Ksh 10,000 sawa na 221,071 kwa kundi la watu wanne, huku VIP ikiwa ni Ksh 9,000, sawa na 1,989,640 za Kitanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles