Kibarua cha Unai Emery matatani

0
729

LONDON, ENGLAND

AJIRA ya kocha wa Arsenal, Unai Emery, ipo matatani baada ya mabosi wa timu hiyo kumtaka kocha huyo kuhakikisha anarudi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Arsenal huu ni mwaka wa tatu mfululizo wanashindwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo wameamua kutumia kiasi kikubwa cha fedha wakati huu wakiangazi kwaajili ya kuboresha kikosi hicho ili waweze kurudi kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Kwa mara ya pili mfululizo Arsenal inashiriki michuano ya Kombe la Euro baada ya kushindwa kufuzu Ligiya Mabingwa Ulaya, huku mashabiki na uongozi wakiwa na kiu ya kutaka kushirik iLigi ya Mabingwa Ulaya.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu Arsenal inashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo nane na kujipatia pointi 15, huku Liverpool ikiongoza msimamo huo wakiwa na pointi 24, wakifuatiwa na mabingwa watetezi Manchester City wenye pointi 16.

Bosi wa timu hiyo, Raul Sanllehi, ameweka wazi kuwa, Arsenal ikimaliza msimu chini ya nafasi nne za juu, haitokuwa na maana yoyote, hivyo kocha huyo anatakiwa kupambana kuhakikisha fedha alizotumia kwaajili ya usajili zirudi kwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

“Nimemwambia Unai Emery kwamba, tumeshindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu kutokana na kutofanya vizuri, lakini msimu huu kutokana na fedha zilizotumika wakati wa usajili wa kiangazi zimeifanya timu hiyo kubwa bora, hivyo tunatarajia kuona inafanya vizuri Ulaya, lakini kama atashindwa kufanya hivyo itakuwa haina maana kwetu,” alisema bosi huyo.

Katika uhamisho wa kiangazi, Arsenal ilitumia kiasi cha pauni milioni 152, ambazo ni zaidi ya bilioni 427 za Kitanzania, kusajili wachezaji sita.

Wachezaji waliosajiliwa na Arsenal wakati wa kiangazi ni pamoja na Nicolas Pepe kwa pauni milioni72, William Saliba pauni milioni 27, Kieran Tierney pauni milioni25, David Luiz pauni milioni 7, Gabriel Martinelli pauni milioni 6 naDani Ceballos pauni milioni 15, hivyo kuwa jumla ya pauni milioni 152.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here