27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Kibali kitolewe kuharakisha utekelezaji mradi wa maji miji 28 – Aweso

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametaka kuharakishwa kwa kibali ambacho Benki ya Exim India inatakiwa kukitoa ili kazi za ujenzi wa mradi wa maji katika miji 28 zianze.

Akizungumza wakati kikao na uongozi wa Benki ya Exim ya India kwa njia ya kieletroniki kuhusu mradi wa maji wa miji 28 amesisitiza uharakishwaji wa utoaji kibali hicho.

Kwa upande wa viongozi wa Benki ya Exim ya India wamekiri kuchelewa kutoa kibali kwa sababu ya mlipuko wa maradhi ya UVICO 19 katika nchi yao hivyo kulazimika kufanya kazi wakiwa nyumbani.

Kikao hicho kilimalizika kwa viongozi wa Benki ya Exim ya India kukubali kuharakisha kutoa kibali ili kazi za ujenzi ziweze kuanza mara moja.

Mradi huo una thamani ya Dola za Marekani milioni 500 na ni moja kati ya miradi mikubwa na wa kihistoria utakaoleta mapinduzi makubwa katika sekta ya maji Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles