31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Khloe aomba kuolewa na mume wake wa zamani

khloe-kardashian-lamar-odomNEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, mdogo wake Kim Kardashian, Khloe, amedai kwamba yupo tayari kuolewa tena na mpenzi wake wa zamani, Lamar Odom.

Wawili hao walikuwa katika ndoa, uhusiano wao ukaingia dosari baada ya Lamar kujihusisha katika matumizi ya dawa za ulevya, hivyo mrembo huyo aliomba kupewa talaka lakini akasitisha mara baada ya kijana huyo kupelekwa hospitali baada ya kuzidisha madawa ya kulevya katika danguro na kupoteza fahamu Oktoba, mwaka jana.

Lakini cha kushangaza, baada ya hali ya Odom kuanza kutengemaa, mwanamitindo huyo akaibuka na kuomba aolewa tena  na mchezaji huyo wa zamani wa kikapu wa timu ya Las Angeles Lakers.

“Naweza kusema sijui nini kinaweza kutokea siku ya kesho, lakini nimejifunza kwamba kama unataka kumchekesha Mungu mueleze mipango yako ya kesho.

“Nilikuwa kwenye uhusiano na Odom na nitaendelea kuwa naye daima bila ya kujali nini kimetokea, ninaamini chochote kinaweza kutokea, bado nina ndoto za kuolewa na yeye na atakuja kunioa tena,” alisema Khloe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,581FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles