27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Tuzo nne zamtoa machozi Adele wa ‘Hello’

AdeleLONDON, ENGLAND

MSANII anayefanya vizuri kwa sasa katika chati za muziki Billboard kutokana na wimbo wake wa ‘Hello’, Adele Adkins, amejikuta akidondosha chozi juzi jukwaani baada ya kupokea tuzo nne za ‘British’ jijini London.

Msanii huyo ameongoza kwa wasanii kutwaa tuzo nyingi katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa 02 uliopo London.

Adele alitwaa tuzo ya msanii bora wa kike, msanii bora wa nchini Uingereza, albamu bora ya mwaka na msanii mwenye mafanikio, tuzo zote zilitokana na wimbo wake huo kufanya vizuri nchi mbalimbali.

“Naomba radhi kwa kudondosha chozi mbele yenu, hii ni kutokana na kutoamini kilichotokea, kutwaa tuzo nne usiku wa leo nimeshindwa kuvumilia hisia zangu.

“Ningependa kutumia nafasi hii kuwashukuru mashabiki wangu wote kwa mchango wenu hadi nimefika hapa na nina furaha isiyoelezeka,” alisema Adele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles