31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rufaa za Blatter, Platini zakataliwa

blatter na platiniZURICH, USWISI

RUFAA iliyowasilishwa kwa kamati ya nidhamu ya FIFA na aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA, Sepp Blatter na Rais wa UEFA, Michel Platini, zimekataliwa.

Viongozi hao wa juu walifungiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa miaka 8, sasa wamepunguziwa na kuwa miaka sita.

Kusimamishwa huko kulifuatiwa na uchunguzi wa kimaadili dhidi yao, hasa baada ya kukumbwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha.

Hata hivyo, viongozi hao wawili walisisitiza hawakufanya makosa yoyote, hivyo walikata rufaa kwa kamati ya nidhamu ya FIFA.

Kutokana na hali hiyo, bado hawakati tamaa na wamepanga kukata rufaa tena katika Mahakama Kuu ya Michezo Duniani.

Blatter, mwenye umri wa miaka 79, amesema hajaridhishwa kabisa na kamati hiyo ya rufaa ya FIFA na lazima asonge mbele.

“Kamati haijatenda haki kabisa kwa jambo hili la kupinga rufaa, lakini bado haijaishia hapo, ni bora nisonge mbele katika mahakama kuu ya michezo,” alisema Blatter.

Wakati huo, Platini amedai kwamba kukataliwa kwa rufaa yake ni sawa na matusi, hivyo hawezi kukubali, lazima achukue hatua ya kwenda mahakama kuu ya michezo.

Platini alikuwa kati ya wagombea urais wa FIFA ambapo uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika leo jijini Zurich, nchini Uswisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles