23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA UKUTA YA LEMA YAKWAMA KUSIKILIZWA

Na JANETH MUSHI-ARUSHA


KESI ya kuhamasisha watu kukusanyika na kufanya maandamano ya Ukuta kinyume cha sheria, inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), imekwama kuendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, baada ya jalada la kesi hiyo kuitwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Juzi kesi hiyo namba 352 ya mwaka 2016, ilipangwa kuendelea kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Benard Nganga.

Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Elizabeth Swai, na utetezi ukiwakilishwa na Wakili Sheck Mfinanga.

Hakimu Nganga alisema jalada hilo lilirudishwa mahakamani hapo baada ya rufaa ya kwanza ya mbunge huyo aliyekuwa akipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kuendelea kusikiliza shauri lake.

Uamuzi wa rufaha hiyo iliyosikilizwa na Jaji Dk. Modester Opiyo wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ilitaka kesi hiyo kurudi kusikilizwa katika mahakama hiyo.

Alisema kwa sasa jalada hilo limeitwa tena Mahakama Kuu ila hawajui iwapo limeitwa kwa rufaa ya pili iliyokatwa na wakili wa utetezi katika Mahakama ya Rufaa Tanzania kupinga uamuzi wa Jaji Dk. Opiyo au laa.

“Jalada limeitwa tena Mahakama Kuu, kwangu linaonyesha liko ‘pending’, sasa lazima nipange tarehe nyingine ili tufuatilie limeitwa kwa ajili gani, kwani limeitwa pamoja na majalada ya kesi nyingine, tutapanga mwezi mmoja ili tujue linaenda Mahakama ya Rufaa au laa,” alisema Hakimu Nganga.

Hakimu Nganga aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 29, mwaka huu itakapotajwa tena.

Mawakili wanaomwakilisha Lema, wanataka kesi hiyo isikilizwe Mahakama ya Katiba (Mahakama Kuu), mbele ya jopo la majaji watatu kutokana na kuwa na masuala ya kikatiba kwenye hati ya mashtaka.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles