24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Kenya yaripoti wagonjwa 123 wapya wa corona

NAIROBI, KENYA

WAZIRI wa Afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe ametangaza watu 123 zaidi kuambukizwa virusi vya corona, katika taarifa yake mpya aliyoitoa jana, Jumatao Mei 27, 2020.

Hiyo ndiyo idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya corona kuwahi kutangazwa kwa siku moja nchini humo tangu ugonjwa huo uingie Kenya mwezi Machi.

Mpaka kufikia sasa Kenya imethibitisha watu 1,471 kuambukizwa virusi hivyo.

Wagonjwa hao wapya wanatokana na sampuli 3,077 ambazo zimepimwa hivi karibuni.

Waziri Kagwe pia alitangaza watu watatu zaidi wamefariki kutokana na corona katika muda wa siku moja na kufanya watu waliopoteza maisha kutokana na virusi hivyo nchini Kenya kufikia 55.

Kati ya wagonjwa hao wapya 123, Jiji la Nairobi linaongoza kwa kuwa na wagonjwa 85 ikifuatiwa na 23 wa Mombasa.

Waziri Kagwe alieleza kuwa ongezeko hilo la wagonjwa linatokana na matumizi ya usafiri wa umma ambao ndio kimbilio la wengi nchini humo.

“Tumegundua kwamba watu wengi wamerejea katika namna ya usafiri wa awali, bila kujali kanuni za kujitenga na kanuni za uvaaji wa barakoa,” alisema.

Waziri Kagwe aliwataka wananchi wa Kenya kuchukua hatua stahiki za kujilinda na kuwalinda watu wengine.

“Haujui unakaa karibu na nani (kwenye gari). Na kulingana na takwimu tunazozipata, nafikiri itakuwa ni salama kudhani kuwa mtu uliyekaa ama kusimama karibu yake kuwa ana corona. Ukishaweka dhana hiyo, hautataka kuivua barakoa yako kwa kuwa utakuwa unajilinda,” alisema.

Kwa mujibu wa Kagwe, japo idadi ya maambukizi imepanda lakini kuna matumaini kwa Kenya. 

“…kwa ujumla wake, idadi hii ya maambukizi ni ndogo ukilinganisha na wengine na hususani idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huu…Utaona ni idadi kubwa ya watu 123 lakini pia utaona idadi kubwa ya watu waliofanyiwa vipimo zaidi ya 3,000,” alisisitiza.

BBC

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles