31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Makatibu wakuu SADC kuondoa vikwazo vya biashara

Mwandishi -Dar es salaam

MAOFISA waandamizi wakiwamo makatibu wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wamependekeza kuruhusu biashara za bidhaa zote kuendelea kusafirishwa katika Nchi zao kama ilivyokuwa kabla ya janga la Virusi vya Corona

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya makatibu wakuu uliofanyika kwa njia ya Mtandao (video conference), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge alisema kuwa mkutano huo umejadili na kutoa mapendekezo ya kuondoa vikwazo vyote vya kibiashara ili kuweza kuendeleza uchumi ndani ya Jumuiya.

Balozi Ibuge alisema kuwa uamuzi huo utawawezesha wananchi kuendelea na maisha yao ya kawaida na biashara zao kwa kuwa janga la COVID 19 litaendelea kuwepo kwa muda ambao ukomo wake haujulikani japo juhudi za kuukabili ugonjwa huo zinaendelea.

“Kikao cha makatibu cha makatibu wakuu cha leo, kimependekeza  kuondoa kikwazo cha bidhaa mahususi tu kupita katika mipaka yetu badala yake bidhaa zote zinazowezesha wananchi wetu kuendelea na maisha ni lazima ziruhusiwe kupita katika mipaka ya nchi wanachama wa SADC,”  alisema Balozi Ibuge.

Aidha, Katibu Mkuu alisema kuwa ni muhimu wa wanaSADC kujumuika katika wakati huu na kuona ni jinsi gani wanaweza kushirikiana na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi wanachama wa SADC unakua kwa kuongeza juhudi katika sekta ya biashara. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles