26.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 24, 2021

Kengele yaibwa kanisani

Nairobi, Kenya

Kanisa la Bikira Maria la Orthodox nchini Kenya inawaomba watu kusaidia kutafuta kengele ya kanisa yenye uzito wa kilo 500 ambayo imeibiwa.

Kanisa hilo lililopo Ngecha eneo la Kiambu, kaskazini mwa mji mkuu wa Kenya, Nairobi, limeviambia vyombo vya habari nchini humo pamoja na polisi kuhusu kuibiwa kwa kengele hiyo.

Waumini wa kidini wamelalamikia kuhusu marufuku ya kusitisha mikusanyiko ya kidini kwasababu ya janga la maambukizi ya virusi vya corona kwani katazo hilo limesababisha wizi kuongezeka makanisani na kuwataka polisi kutoa ulinzi.

Kanisa limesema pia limepoteza chupa 10 za mvinyo , vifaa vya matangazo ya nje na vitu vingine hata kabla ya kuibiwa kwa kengele hiyo ya shaba.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,967FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles