23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Corona yazidi kutikisa India

-Delhi

Idadi ya jumla ya visa vya ugonjwa wa Covid-19 nchini India imepindukia milioni 18 leo baada ya kutolewa rekodi nyingine ya dunia katika idadi ya maambukizi kwa siku.

Data za wizara ya afya ya India zinaeonyesha visa vipya zaidi ya 379,257 na vifo vipya vya watu 3,645 vilivyorekodiwa leo na ndiyo idadi kubwa zaidi ya vifo kuripotiwa kwa siku nchini humo tangu kuanza kwa janga hilo.

India inatarajia kupokea mashine 550 za kutengeneza hewa ya oksijeni kutoka kote duniani wakati msaada ukianza kuingia nchini humo.

Tayari ndege mbili kutoka Urusi, zilizobeba mashine 20 za kutengeneza oksijeni, mashine 75 za kusaidia kupumua, kompyuta 150 za vyumba vya wagonjwa na tani 22, zimewasili New Delhi.

Marekani inapeleka msaada wa hadi dola milioni 100, ikiwemo mitungi 1,000 ya oksijeni, barakoa milioni 15 na vifaa milioni 1 vya kufanyia vipimo vya kasi vya corona.

Ujerumani inapeleka India mashine 120 za kusaidia kupumua na kisha baadae kiwanda kinachohamishika cha kutengeneza oksijeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles