Kayala kutumbuiza nchini Kenya Aprili 16

0
652

kayalaa,NA GLORY MLAY

MWIMBAJI anayetamba na albamu ya ‘Maajabu ya Damu ya Yesu’, George Kayala, anatarajiwa kwenda nchini Kenya kutumbuiza katika tamasha maalumu litakalofanyika Aprili 16, mwaka huu Ukumbi wa Catholic University of Eastern Africa jijini Nairobi nchini humo.

Kayala alipata mwaliko wa kuhudhuria na kutumbuiza katika tamasha hilo linaloitwa Dreams Come True kutokana na kukubalika kwa ubora wa nyimbo zake zilizopo katika albamu yake ya pili.

“Mwaliko huu ni faraja kwangu kwani kitendo cha kwenda Nairobi kuhubiri injili kwa njia ya uimbaji ni kutimiza andiko lisemalo ‘Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri injili’ na huu ni mwanzo wa kwenda mataifa mengine kwa nje na Afrika Mashariki,” alisema Kayala.

Tamasha hilo hufanyika Aprili na Agosti likishindanisha waimbaji na waigizaji wanafunzi wa shule na vyuo mbalimbali nchini Kenya na washindi huendelezwa kisanaa na kulipiwa ada za masomo na kampuni ya Afrika Nasaha ya nchini humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here