29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Baby Madaha: Dubai kumenichelewesha sasa narudi upya

babyNA SUZANA MAKORONGO

BAADA ya kimya kirefu msanii mwenye vituko lukuki, Baby Joseph, ameibuka na kudai kwa sasa atakuwa na kampuni itakayokuwa na jukumu la kusimamia muziki wake na wa wasanii wengine ili kuuendeleza muziki huo kwa njia nyingine tofauti na alivyokuwa akifanya mwanzo.

Mkali huyo aliyetokea Bongo Star Search alisema ujio wake mpya utaanza baada ya filamu zake mbili ambazo zitatoka mwishoni mwa mwezi ujao.

“Nitakuja kivingine hadi Aprili nitafanya uzinduzi mkubwa kwa ajili ya ujio huo nitatambulisha kampuni yangu itakayokuwa na kazi ya kusambaza kazi zangu za filamu na nyimbo lakini pia kusimamia kazi za wasanii wengine,” alisema Baby Madaha.

Madaha alisema kimya chake kingi pia kilitokana na safari yake ya Dubai ambayo ndiyo imemfanya aweze kuzindua kampuni hiyo ya kusimamia kazi zake na wasanii wengine pamoja na kuendeleza muziki kwa ujumla kwa kusaidia wasanii wanaochipukia.

“Nilikuwa Dubai wengi wanajua nimeolewa lakini sijaolewa nipo na shughuli zangu na kama nikiolewa nitaweka wazi suala hilo, kwa sasa natakamilisha ujio wangu mpya wa kampuni na si vinginevyo,” aliongeza Madaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles