Cool J atangaza kustaafu muziki

0
772

Cool JNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki nchini Marekani, James Smith (Cool J), amedai anatarajia kustaafu muziki baada ya kuachia albamu yake mpya.

Msanii huyo amedai anatarajia kuachia albamu mpya ambayo amemshirikisha mkali wa muziki huo, Eminem na kisha kustaafu muziki.

Hata hivyo, wiki iliyopita aliweka wazi kwamba amestaafu muziki, lakini amewashangaza mashabiki wake kutokana na kauli yake kwamba atastaafu rasmi baada ya kuachia albamu hiyo ambayo hadi sasa bado haina jina.

“Naweza kusema tayari nimestaafu muziki, lakini nitastaafu rasmi baada ya kuachia albamu yangu, kwa sasa siwezi kufanya tena muziki nasimamia albamu hiyo, lakini baada ya kuiweka sokoni utakuwa mwisho wa muziki wangu,” alisema Cool J.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here