24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

The Game amaliza tofauti zake na 50 Cent

The GameNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki wa hip hop, Jayceon Taylor (The Game), amemaliza tofauti zake na nyota mwenzake, 50 Cent, baada ya The Game kuisifia pombe ya vodka ambayo inamilikiwa na kiongozi huyo wa G. Unit.

The Game alikuwa hana uhusiano mzuri na kundi hilo la G.Unit, lakini siku za hivi karibuni aliweka picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa na msanii, Lloyd Banks, anayetoka katika kundi linaloongozwa na 50 Cent.

Kikubwa ambacho kimewachanganya mashabiki ni baada ya kuona msanii huyo akiweka picha nyingine akiwa anakunywa pombe aina ya vodka na kuanza kumsifia 50 Cent kutokana na kinywaji hicho.

“Vodka ni kinywaji kizuri na kina ubora, naweza kuendelea kukitumia bila kujali vyombo vya habari vitasema nini. “Mwaka huu nimeamua kuja kivingine, sina ugomvi na mtu ila nina ugomvi na fedha kwa kuwa nazitafuta kila siku,” aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles