27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

Kavumbagu anusurika kifo Dar

AZAMWEBKAVUNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI mahiri wa klabu ya soka ya Azam FC, Didier Kavumbagu, jana amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya eneo la Mtoni Kijichi kufuatia gari lake kugongwa na kupinduka.

Kavumbagu alipata ajali hiyo akiwa njiani kuelekea Hospitali ya Mikocheni kumuona daktari anayemtibu tangu alipopata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar.

Akizungumza na MTANZANIA, Kavumbagu alisema kwamba ilikuwa bahati kwake kunusurika kwenye ajali hiyo iliyotokea saa 2:00 asubuhi ambayo ilisababisha gari lake kutumbukia mtaroni.

“Ajali ilitokea wakati nikiwa naenda Mikocheni hospitali kwa ajili ya matibabu, kutokana na majeruhi yangu ya kifundo cha mguu mara ghafla nililiona gari likitokea sheli na kunigonga ubavuni na kunisukumiza hadi pembeni ambako kulikuwa na roli la taka.

“Niligongana na gari la kubebea taka na kuingia mtaroni, hata hivyo nilishukuru baada ya kutoka salama kwenye gari hilo,” alisema Kavumbagu.

Mbali na ajali hiyo, Kavumbagu alisema kwa mujibu wa daktari wake, anatarajia baada ya wiki moja ataanza mazoezi mepesi ili kurejea kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Nakaribia kurejea kwenye ligi muda mfupi ujao, hivyo nawataka mashabiki wangu kuwa na subira na kuniombea niweze kuwa na afya njema,” alisema Kavumbagu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles