22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

KAULI YA RAIS MAGUFULI YAMTIKISA MAKONDA

Na AGATHA CHARLES – DAR ES SAALAM


KAULI ya Rais Dk. John Magufuli kuwa Jiji la Dodoma ndilo linaongoza kwa mapato nchini imeonekana kumtikisa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambaye amempa maagizo Katibu Tawala (RAS), Abubakar Kunenge, kutafuta sababu za kushuka huko.

Makonda alitoa kauli hiyo jana, wakati wa hafla ya kuwakaribisha wakuu wa wilaya wapya na kuwaaga waliohamishwa vituo vyao vya kazi, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Makonda alimwelekeza Kunenge kukutana na wakurugenzi wa halmashauri zote za jiji hilo kupitia taarifa za mapato ili kubaini sababu za Dar es Salaam kupitwa na Dodoma katika ukusanyaji wa mapato.

“Tuongeze vyanzo vya mapato na kusimamia taarifa za mapato…RAS pamoja na wakurugenzi pitieni taarifa za kila manispaa Mkoa wa Dar, na kuangalia kwanini tumeshuka, na kama tumeshuka ni vigezo gani, nini kimetufanya tukashuka Dodoma ikapanda. Haiingii akilini kuwa sisi kweli tukazidiwe na Dodoma. Tutafanya kadri iwezekanavyo turudi kuongoza kama awali. Kwa hiyo RAS nategemea mazuri kutoka kwako,” alisema Makonda.

Mbali na eneo hilo, Makonda alimtaka RAS huyo kufanyia kazi kitengo cha ardhi, ambacho alisema ni moja ya idara zilizokuwa mzigo.

“Anza na kitengo cha ardhi, kuanzia ngazi yangu ya mkoa kina migogoro mingi ambayo hakijaweza kuitatua. Yuko mkuu wao wa idara hapo ofisini kwangu ni mzigo tena wa msumari. Sina furaha, tulivyoitisha migogoro ya wananchi waliodhulumiwa na kunyanyasika ni zaidi ya 10,000. Migogoro ilikuwa ni mingi, lakini namba moja ni ardhi,” alisema Makonda.

Makonda alisema kitengo cha sheria kilifanya kazi ya uchambuzi kuhusua aina ya migogoro na ukakamilika na kukabidhiwa kila idara, lakini hadi sasa hakuna majibu.

“Kuna taarifa za uongo, fuatilia, mimi nilishapewa taarifa za uongo mara saba. Mfano taarifa ya World Bank ilikuwa ya uongo, ilifikia kipindi nilikuwa situmii taarifa za RAS,” alisema Makonda.

Alisema Septemba mwaka huu kutakuwa na ziara ya Dar es Salaam mpya itakayotanguliwa na wakuu wa wilaya, kisha Mkuu wa Mkoa huyo, RAS aunde kamati ya kukagua mali za mkoa wa Dar es Salaam.

Inaendelea……….. Jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA JUMAMOSI

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles