23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu Mtendaji AFCFTA kuzindua Sabasaba

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

KATIBU Mtendaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AFCFTA), Wamkele Mene anatarajiwa kufungua maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) Julai 3, 2022.

Hayo yamebainishwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashantu Kijaji alipotembelea katika viwanja vinapofanyika maonesho hayo maarufu kama sabasaba yaliyoanza Juni 28, mwaka huu.

Alisema Septemba, mwaka jana Bunge lilipitisha mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika na Januari, mwaka huu ilipelekwa taarifa ya kuonesha utayari wa Tanzania kuingia katika eneo hilo la biashara.

“Kawaida wananchi walizoea maonesho yanazinduliwa na kiongozi wa nchi lakini mwaka huu itakuwa ni tofauti, Rais wetu Samia Suluhu Hassan alitoa fursa kwa sisi Watanzania kumkaribisha Katibu Mtendaji huyu na haya ni matokeo ya sisi kuingia huko katika mashirikiano,” alisema Dk Kijaji.

Aliwataka wafanyabiashara waanze kuzalisha biashara kwaajilu ya soko la Afrika na sio Tanzania pekee.

“Tunakoelekea ni kwamba Afrika inataka kuwa soko huru ambapo biashara zitatoka nchi moja kwenda nyingine bila vikwazo vyovyote. Tulichokubaliana katika mkataba huo ni kwamba kila nchi iangalie sifa zipi za kipekee ambazo zikiweza kuchukuliwa na kutumiwa vizuri ndani ya Taifa hilo tunaweza kuzalisha kwa gharama nafuu na kuweza kuuza bidhaa zetu nje ya nchi.

‘”Na ndio maana mmeona wawekezaji wengi wanakuja nchini kwetu na hata Katibu Mtendaji huyu anakuja kuwaambia Watanzania Afrika tunakwenda kuwa soko moja, bidhaa zinazozalishwa Tanzania ziuzwe Afrika nzima,” aliongeza.

Vilevile aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa maonesho hayo ambayo alisema yamefana kwa asilimia 97.

“Tujitokeze kwa wingi kuja kumsikiliza mgeni wetu rasmi ambaye atatuekeza fursa mbalimbali zilizopo katika soko hilo ili tuweze kuzitumia kwani tumerahisishiwa,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles