23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Meridianbet Waanzisha Shindano la Mikwaju ya Penati Kuisaidia Jamii

Meridianbet inaendesha shindano la upigaji wa mikwaju yake penati kwa ajili kuchangisha fedha ambazo lengo la ukusanyaji wa fedha hizo likiwa ni kurejesha kwa Jamii. Kampuni hii ambayo ni wakongwe na magwiji wa ubashiri wa michezo na kasino ya mtandaoni, wamekuwa wakifanya shughuli mbali kama hizi zinazowaweka karibu zaidi na Jamii.

Wakati huu Kampuni imeamua kuwatumia watu maarufu na wahamasishaji kuichangia Jamii, ambapo mashuti ya penati yanatoa thamani ya mchango ambao mtu huyu anayepiga anaisaidia Meridianbet kuichangia Jamii. Kila shuti linalofikia nyavu limepewa thamani ya TSH 50,000. Baada ya kushinda mashuti kadhaa kati ya mikwaju mitano anayotakiwa kupiga, mhamasishaji anachagua kundi gani la jamii lisaidiwe kwa fedha hizo.

Wakiwa na balozi wao, na mhamasishaji Jemedari Saidi Kazumari aliyepiga penati 5 na kupata 4 kati ya hizo na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi laki 200,000/=. Jemedari alipendekeza fedha hizi zipelekwe kwenye taasisi ya tiba ya CCBRT.

Meridianbet iliwasilisha fedha hizo CCBRT, ambao walitoa utaratibu sahihi wa kupekela kiasi kile kwa walengwa ambao ni watu wanaohitaji huduma za kitabibu hospitalini hapo.

Uongozi wa CCBRT ulielekeza kiasi hicho kwenye matibabu ya mtoto Agness Elias aliyepaswa kufanyiwa upasuaji wa miguu ambao gharama za upasuaji na matibabu ya kiasi cha 250,000/=.

Viongozi kutoka Meridianbet waliongeza fedha zaidi ili kukidhi gharama za matibabu, kiasi cha shilingi elfu 50,000/= kikiongezwa kwenye shilingi 200,000/= iliyopatikana awali kwa mikwaju ya penati nne alizoshinda jemedari, kukamilisha shilingi 250,000/= kwa ajili ya matibabu.

Pia, Meridianbet waliongeza kiasi kingine cha shilingi 250,000/= kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya shule na chakula kwa kipindi ambacho ataendelea kuuguzwa akiwa nyumbani.

Mama mlezi wa mtoto Agness, Bi Calorine ameishukuru Meridianbet kwa kuweza kumsaidia binti yake kupata matibabu na zaidi ameiomba inedelee na moyo wa kusaidia watu wanaohitaji msaada katika jamii na kwa namna hiyo itagusa maisha ya wengi wanaohitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles