25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Kanye West ageukia muziki wa Injili

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Kanye West, ametangaza nia ya kutaka kuachana na muziki huo na kumtumikia Mungu kwa nyimbo za Injili.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 42, alianza kujulikana kwenye muziki tangu mwaka 1996, akifanya hip hop, lakini sasa ameweka wazi kuwa ni wakati wa kumtumikia Mungu kwa kufanya muziki wa Injili katika maisha yake yaliyobaki.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Jesus Walkes, aliyasema hayo juzi wakati anaelezea sababu za kuchelewesha ujio wa albamu yake mpya ya Jesus Is King, ambayo ilitakiwa Ijumaa ya wiki iliopita.

“Nimefanya makubwa kwenye muziki ambao hauna maneno ya Mungu, lakini sasa ni wakati wa kuachana na muziki huo na kugeukia Injili hadi mwisho wa maisha yangu,” alisema msanii huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles