Huddah athibitisha Diamond, Tanasha kupata mtoto

0
1200

NAIROBI, KENYA

STAA wa mitindo nchini Kenya, Huddah Monroe, ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuanika ujumbe mfupi wa maandishi waliowasiliana na mpenzi wa Diamond Platnumz, Tanasha Donna ukionesha kuwa mrembo huyo tayari amepata mtoto.

Diamond na Tanasha wameamua kufanya siri kwa mashabiki zao hadi hapo watakapoamua kuweka wazi, lakini Huddah ambaye amekuwa rafiki wa karibu na Tanasha ameweka wazi kutokana na mawasiliano yao.

Hudddah alimuuliza Tanasha lili atajifungua mtoto wake? Tanasha akajibu tayari amejifungua na mtoto huyo anamsubiri shangazi yake kuja kumtembelea.

Huyo ni mtoto wa kwanza kwa Tanasha, lakini ni mtoto wa nne kwa Diamond. Watoto wawili alifanikiwa kuwapata na Zari Hassan kutoka Uganda, huku mmoja akimpata na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here