The Rock, Vin Diesel wamaliza ‘bifu’ lao

0
1492

NEW YORK, MAREKANI

STAA wa filamu nchini Marekani Dwanye Johnson maarufu kwa jina la The Rock, ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mgogoro na rafiki yake Vin Diesel.

Msanii huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuwashukuru mashabiki zake ambao walikuwa wanataka bifu hilo limalizike ili waendelee na kazi zao kama ilivyo kwenye filamu ya Fast & Furious.

“Napenda kutumia nafasi hii kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki wote ambao walikuwa wanataka tuweke pembeni tofauti zetu, kutoka kwa mashabiki jambo hilo limefanikiwa na sasa hakuna tofauti kati yetu, urafiki kama kawaida.

“Namshukuru Vin Diesel kwa sapoti yake kwa kuwa yeye ndiye aliyenifanya niwe kwenye familia ya Fast & Furious, yeye ni kama kaka yangu acha maisha yaendelee,” alisema The Rock.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here