25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Kanyasu atoa msimamo malikale za majini

– MALINDI

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa msimamo kuwa Tanzania ipo tayari kuridhia mkataba wa mwaka 2001 kwa nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuhusu uhifadhi wa urithi wa utamaduni wa majini kama masharti iliyoyatoa yatatekelezwa.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kikanda wa uhifadhi wa urithi wa utamaduni uliomo majini uliofanyika mjini Malindi nchini Kenya juzi, Waziri Kanyasu alisema mkataba huo utahusu utafutaji wa malikale zilizomo majini zikijumuisha miji iliyozama (sunken cities), meli, ndege, vipande vya vyungu, sarafu, mashua na boti.

Waziri Kanyasu aliitaka UNESCO iwajengee uwezo wataalamu wa uhifadhi wa urithi wa utamaduni uliomo majini ili waweze kubaini na kuweka kumbukumbu za maeneo yote yenye malikale hizo.    

Alisema Tanzania inahitaji kujifunza kutoka nchi nyingine zilizoridhia mkataba huo na kuimarisha mashirikiano kati ya nchi zilizoridhia na ambazo hazijaridhia ili kubadilishana uzoefu na utaalamu.

Alitaka mkataba huo uzingatie masilahi mapana ya nchi ili usizuie uvunaji wa rasilimali nyingine kwenye eneo ambalo lipo katika mkataba.

Mkutano huo ulihudhuriwa na mawaziri kutoka nchi za Tanzania, Comoro, Djibouti, Ethiopia, Madagascar, Shelisheli, Somalia, Afrika Kusini, Rwanda, Eritrea na Kenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles